Aunt Ezekiel Atumbuliwa Jipu Na Serikali Ya Magufuli, Ipo Hapa



Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.

Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.



Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Aunt kutaka kujua kisa kamili ambapo alipobanwa alikiri kukamatwa kwa gari lake hilo kwa makosa ya kukwepa kodi wakati linaingizwa Bongo hivyo kuwa mikononi mwa TRA.

“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.

“Nilishtuka sana baada ya kukamatwa kwani nilihisi ndiyo mwisho wa kuwa na gari langu lakini sasa nimepata moyo baada ya kuambiwa hakuna kilichochakachuliwa.


“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’ huku akigoma kutaja bei yake.

-GPL

Haya Ndio Maisha ya Mbunge SUGU Kwa Dasa


Kwenye Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 na 2015, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu alijishusha na kujinyongesha ili wananchi wamwamini na kumpa kura. Miongoni mwa mambo aliyotumia kuombea kura ni kutomiliki Magari na Nyumba za Kifahari na badala yake atatumia fedha atakazopata kuwahudumia wananchi hasa kwenye huduma za Afya na Elimu. Moja ya ahadi kuu ya Mr Sugu ni hii hapa na nanukuu;

========="Nikichaguliwa kuwa Mbunge, sioni faida ya kutembelea magari ya kifahari na kulala kwenye jumba la kifahari wakati wananchi wangu wanateseka kwa kukosa huduma bora hospitalini na watoto wanakosa vitabu, vyumba vya madarasa na madawati. Nitauza mpaka gari la Mkuu wa Mkoa ili kuhudumia Jamii========= Mwisho wa Kunukuu.

Sasa linganisha kauli hiyo na haya maisha anayoishi Mbunge wa Mbeya Mjini, Mr Sugu. Je kwa tafsiri yako msomaji, nini maana ya Magari ya Kifahari na Nyumba ya kifahari? Hivi anavyomiliki Sugu si vitu vya kifahari?

Jack Wolper Adaiwa Kutolewa vyombo nje na Mwenye Nyumba......

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ambaye hivi karibuni ameonekana kulegalega amedaiwa kutolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Mikocheni jiji Dar.
Chanzo chetu makini kabisa kinadaiwa kuwa kipindi staa huyo akiwa nchini Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini kwa kushindwa kulipia kodi kwa kipindi kinachotakiwa, kabla hata hajarejea mwenye nyumba aliamua kutoa vitu nje na ndugu wa staa huyo kila mmoja kuelekea anakokujua.

“Maskini, wakati Wolper yupo Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini ilishindikana kulipa kodi hivyo mwenye nyumba aliwatimua ndugu zake,” kilisema chanzo hicho.
Kilizidi kufunguka kuwa, baada ya Wolper kurejea nchini ilibidi kuishi hotelini mpaka sasa ili kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kupanga nyumba ambayo ataweza kuishi pamoja na ndugu zake.

“Wolper na mpenzi wake tangu waliporejea nchini wanaishi hotelini, nafikiri wanajipanga ili waweze kupata fedha za kuweza kupanga tena nyumba kama ilivyokuwa huko nyuma,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Wolper kwenye simu ambapo alipoulizwa kama ni kweli ametolewa vitu nje, alijibu;

“Hao wanaosema nimefulia hadi kutolewa vitu nje ni wazushi tu, hawana nia njema na mimi, najua ninachokifanya mjini hivyo hawanipi shida, wache waseme mpaka wachoke.”

MPYA Kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart)...Tarehe ya Kuanza Kazi Yatajwa Rasmi...

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.

Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Simbachawene alisema baada ya kukutana na wadau wa mradi huo, wamewahakikishia kuwa utaanza rasmi mwezi ujao bila kukosa.

“Tumeambiwa mradi huu una mikataba mingi na kuwa bado kuna mjadala mkubwa wa mikataba. Hatuwezi kulazimisha maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya, hivyo tunaendelea na mijadala ya mikataba,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza alisema wameutembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua tatizo linaloukwamisha kuwa ni fedha na kuitaka Serikali kutoa fedha ili uanze.

Aliesema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kupunguza kero ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaokabiliwa na tatizo la usafiri na foleni za barabarani, hivyo kutumia muda mrefu barabarani.

Rweikiza alisema kukamilika kwa mradi huo na kuanza kufanya kazi kutapunguza kero na kuokoa muda mwingi uliokuwa ukitumia bila uzalishaji.

Tuhuma za Mwanamuziki TID Kutumia Madawa ya Kulevya...Mwenyewe Afunguka

Baada ya KR kujitambulisha kuwa yeye ndiye Rais wa RADA Entertainment na Juma Nature kumpinga kwa kejeli akisema hamtambui Rais yoyote zaidi ya Rais Magufuli hatimaye TID anyoosha maelezo.


T.I.D amesema muda ukifika watamuapisha rasmi KR Mulla kuwa Rais wa Radar Entertainment na kutoa sababu za kufanya kazi na KR Mulla katika label yake.

Zaidi eNews ilipotaka kupata maelezo ya kina juu ya tuhuma za TID kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, TID aligoma kusema chochote, na hata alipoulizwa juu ya tuhuma hizo kwa wasanii wengine pia TID alisema “Muda ukifika nitaongea nyie endeleeni kuongea vitu msivyovijua”.

Manispaa ya Kinondoni Chini ya CHADEMA Yatangaza Neema Kwa Wakazi Wake..Sasa Kila Mkazi Kupata Bima ya Afya

Manispaa  ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inayoongozwa na Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya Ukawa imeanza kazi kwa staili ya aina yake baada ya kutangaza neema ya bima ya afya kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

Imeahidi kuanzisha mpango maalum ambao kila mwananchi wa Manispaa hiyo atachangia Sh. 40,000 kwa mwaka ili aunganishwe na mpango wa matibabu wa bima ya afya ambao utawawezesha kupata matibabu ya bure katika hospitali mbalimbali.

Mpango huo utaanza kutekelezwa mwezi Juni mwaka huu, huku bajeti ya Manispaa hiyo ikiongezeka kwa asilimia 59 kutokana na kukua kwa mapato ya ndani.

Wazee wa Manispaa hiyo nao wametangaziwa neema ya matibabu bure kwani watapewa kadi maalum zitakazowawezesha kutibiwa hospitali za umma.

Mapato hayo yametokana na ukusanyaji madhubuti katika kodi za majengo, mabango, leseni za biashara, huduma za kuegesha magari, hoteli na ruzuku ya serikali kuu.

Bajeti ya mwaka 2016/2017 katika Manispaa hiyo inafikia Sh. Bilioni 248.47 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana ambayo ilikuwa ya Sh. Bilioni 156.24.

Katika bajeti ya mwaka huu kuna ongezeko la Sh. zaidi ya bilioni 92.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob aliwasilisha bajeti hiyo jana jijini Dar es Salaam katika kikao cha Baraza la Madiwani.

Baada ya kuwasilisha bajeti hiyo, Madiwani wote wakiwamo wa upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliipitisha kwa kauli moja ili ianze kuwahudumia wananchi.

Akisoma bajeti hiyo, Jacob alitaja ukusanyaji wa mapato ya ndani umeingiza Sh. bilioni 64.28 na kwamba imeongezeka kutoka Sh. bilioni 56.6 za mwaka jana.

Licha ya bajeti ya mwaka huu kulenga kugharamia huduma za matibabu, lakini imelenga kujenga shule ya bweni katika Kata ya Goba kwa gharama ya Sh. milioni 250, ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule, kujenga vyumba vya madarasa na ununuzi wa madawati 30,000.

Kazi nyingine zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa Barabara kuelekea kituo cha daladala cha ya Simu 2000 na Barabara ya Akachube ambazo zimetengewa Sh. bilioni 50.

Kuhusu suala la usafi, Meya Jacob alisema kila Kata itakuwa na gari lake la kuzolea takataka na Manipaa imetenga Sh. 2.2b .

Manispaa hiyo ina jumla ya Kata 25 na Sh. bilioni 3.6 zimetengwa kwa ajili ya gharama za kusafirisha takataka.

Aidha, katika bajeti hiyo, Manispaa inatarajia kununua Trekta lenye kijiko kwa ajili ya kutengeneza barabara na zimetengwa Sh. bilioni 1 kwa ajili ya kazi hiyo.

Kazi nyingine za fedha hizo ni kuweka sakafu ngumu katika masoko yote ya manispaa, ili kuondoa adha ya uchafu na matope katika msimu wa mvua na zimetengwa Sh. bilioni 1.65.

Kuhusu vijana na wanawake Manispaa hiyo imetenga Sh. bilioni 4.7 kwa ajili ya kuwakopesha na kila Kata itapata Sh. milioni 200.

LEMUTUZ Afunguka Kuhusu Kijana Aliyekamatwa Arusha Kwa Kumwita Rais Bwege..Ailaumu Serikali na Polisi

 Blogger Lemutuz naye amefunguka kuhusu kijana aliyekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kutumia Mtandao wa Facebook kumwita Rais Magufuli Bwege  na kwamba hawezi kufananishwa na Nyerere..

Lemutuz Kayasema Haya..... 
lemutuz_nation Mr. Isaack Jana Arusha akirudishwa Rumande baada ya kushitakiwa na Serikali kwa kumtukana Rais Magufuli kwenye mitandao ya kijamii ....hapa ndipo ninapoilaumu Polisi na Serikali I mean huyu mtu kamtukana Rais juzi tu Jana tayari Mahakamani kwa nini iwe hivyo na kwa wananchi wa Kawaida? ....Sheria ipo now kama kuna njia rahisi ya kuwakamata hawa Cyber Abusers ni kwa nini wanapotukanwa Wananchi wa Kawaida inakuwa almost kama hamna Sheria wala uwezekano wa kuwakamata lakini akitukanwa Rais Mara moja wanapatikana? ....ndio maana ninasema na sisi Wananchi tusimameni tuhesabiwe tukatae hawa watu kutuvurugia amani kwenye Social Media .....tupambane nao hata kama itachukua muda mrefu lakini wapate ujumbe kwamba sio Wananchi wote tupo tayari kuwapa hiyo nafasi tutawatafuta na watafikishwa kwenye Sheria tu hata kama ni Miezi SITA au Mwaka wa kuwatafuta! - le Mutuz 34min

Kategori

Kategori